Kenya yaadhimisha miaka 10 tangu kutokea shambulio la kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa, ambpo wanafunzi 147 waliuwawa katika tukio hilo. Jacob Safari amezungumza na Kalekye Mwandikwa, mama aliyempoteza mwanawe aliyekuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Garissa. Mwandikwa ameelezea jinsi alivyopokea taarifa ya shambulizi hilo.