JangaUjerumani
Mhamiaji akamatwa mkasa wa gari kuparamia watu Munich
14 Februari 2025Matangazo
Kwenye mkasa huo ambao viongozi wa Ujerumani wameutaja kuwa "shambulizi" watu 30 wamejeruhiwa na baadhi yao wako kwenye hali mahututi.
Inaarifiwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Afghanistan alifanya tukio hilo mnamo majira ya asubuhi katikati ya mji wa Munich akiulenga mkusanyiko wa watu waliokuwa wakishiriki maandamano ya chama cha wafanyakazi.
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amekitaja kisa hicho kuwa "cha kuchukiza" na kuahidi hatua kali dhidi ya waomba hifadhi wanaofanya uhalifu.
Amesema serikali yake itaharakisha mchakato wa kuwarejesha makwao watu wasio na uraia wa Ujerumani na wanaofanya makosa ya jinai. Ameahidi mshukiwa wa mkasa wa Munich ni miongoni mwa wale watakaorejeshwa kwenye mataifa yao.