Mhafidhina Karol Nawrocki ashinda urais Poland
2 Juni 2025Viongozi mbali mbali barani Ulaya wamempongeza mgombea wa upinzani wa chama cha siasa za kizalendo nchini Poland Karol Nawrocki baada ya kutangazwa mshindi leo Jumatatu wa matokeo ya uchaguzi wa rais.
Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ni miongoni mwa viongozi waliompongeza.
Ushindi wa Nawrockikutoka chama cha sheria na haki aliyepata asilimia 50.89 ya kura ni pigo kubwa kwa juhudi za serikali ya siasa za wastani za kuimarisha mwelekeo wa Poland wa kuunga mkono Umoja wa Ulaya.
Mwanasiasa huyo huenda akatumia kura yake ya turufu kama rais kuzima mwelekeo wa sera za kiliberali wa waziri mkuu Donald Tusk. Rafal Trzaskowski kutoka muungano tawala , aliyepambana dhidi ya Nawrocki kwenye uchaguzi wa jana alipata asilimia 49.11.