Mgomo wasababisha kufungwa uwanja wa ndege wa Hamburg
9 Machi 2025Msemaji wa uwanja wa ndege wa Hamburg amesema kutokana na mgomo huo, ndege 144 zilizopaswa kuwasili na 139 zilizotakiwa kuondoka Jumapili zimefutwa na uwanja huo wa ndege umefungwa.
Mgomo huo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi cha Verdi ulipaswa kuanza Jumapili jioni na kuhitimishwa Jumatatu usiku.
Soma pia: Wafanyakazi wa reli, viwanja vya ndege wagoma tena Ujerumani
Chama hicho kinawataka wafanyakazi wake katika viwanja 13 vya ndege vya Ujerumani kufanya mgomo Jumatatu kabla ya awamu nyingine ya mazungumzo kati ya serikali ya shirikisho na wafanyakazi yaliyopangwa kufanyika mwezi Machi.
Ni Hamburg pekee ndiyo iliyouanza mgomo mapema Jumapili. Msemaji wa Verdi amesema mgomo wa mapema wa Hamburg ambao haukutangazwa ni muhimu ili kuhakikisha athari za mgomo zinashughulikiwa.