Wakili wa Kenya Martha Karua afukuzwa Tanzania
19 Mei 2025Wakili na mgombea urais wa zamani nchini Kenya, Martha Karua, amesema amefukuzwa kutoka nchini Tanzania ambako alipanga kuhuduria kusikilizwa kwa kesi dhidi ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani anayekabiliwa na mashitka ya uhaini.
Karua, waziri wa zamani wa sheria wa Kenya, ambaye amekuwa msitari wa mbele kupiga kelele kuhusu kurudi nyuma kwa demokrasia Afrika Mashariki alisema jana Jumapili kufukuzwa kwake ni ishara kwamba mamlaka za Tanzania hawataisikiliza kesi na kutoa hukumu ya haki kwa kiongozi wa upinzani wa chama cha Chadema Tundu Lissu.
Mwanasiasa maarufu wa Kenya Karua akamatwa Tanzania
Karua alisafiri kwenda Dar es Salaam kushuhudia na kufuatilia kesi ya Lissu ambaye anatarajiwa kupandishwa kizimbani leo Jumatatu kwa mashitaka ya uhaini ambayo hukumu yake inaweza kuwa na adhabu ya kifo.
Karua alisema yeye na kundi lake walizuiwa walipowasili uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kutiwa kwenye ndege kurudishwa Kenya siku hiyo hiyo.