SiasaColombia
Colombia: Mgombea afariki miezi miwili baada ya kushambuliwa
12 Agosti 2025Matangazo
Licha ya dalili zilizoleta matumaini katika wiki za hivi karibuni, madaktari walitangaza kuwa mwanasiasa huyo alianza kuvuja damu kwenye ubongo siku ya Jumamosi.
Mnamo Juni 7, 2025, Uribe aliyekuwa Seneta wa kihafidhina mwenye umri wa miaka 39, alipigwa risasi za kichwa na kwenye mguu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mji mkuu Bogota.
Washukiwa sita wanaohusishwa na shambulio hilo walikamatwa, akiwemo mshambuliaji anayetajwa kuwa kijana mwenye umri wa miaka 15. Kifo cha mgombea huyo ambaye angelichuana na rais Gustavo Petro katika uchaguzi wa hapo mwakani, kimezusha hofu ya kuiona Colombia ikirejea katika ghasia za kisiasa.