Mgogoro wa Pakistan na India waongezeka
5 Mei 2025Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ameakhirisha ziara yake ya kiserikali ya Malaysia, chini ya kiwingu cha kuongezeka mivutano na hali ya wasiwasi kati ya nchi yake na India.
Hatua ya kuakhirishwa ziara hiyo iliyotarajiwa kuanza Ijumaa, imetangazwa na waziri mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim leo Jumatatu.Soma pia:Pakistan yafanya jaribio la pili la kombora la masafa marefu
Kufuatia mvutano kati ya mataifa hayo mawili ya Nyuklia barani Asia, waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi amewasili Islamabad leo akiwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea Pakistan tangu ulipozuka mvutano katika jimbo linalozozaniwa la Kashmir.Soma pia: India yataka washambuliaji wa Kashmir wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria
Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya Tehran kujitolea kusaidia kuwa msuluhishi kati ya India na Pakistan.
Araghchi atakutana na mwenzake Ishaq Dar,pamoja na rais Asif Zardari na waziri mkuu Shehbaz Sharif. Wakati huohuo jeshi la Pakistan limefanya jaribio la pili la kombora tangu ulipoanza mvutano huo mpya na India.