Mgogoro wa Kongo kuugubika mkutano wa kilele wa AU
12 Februari 2025Matangazo
Kando na mzozo wa Kongo utajadili pia hatua ya Marekani ya kuondoa misaada ya kiutu.
Mkutano huo wa Kilele unawakutanisha wakuu wa mataifa ya Umoja huo unaokaliwa na karibu watu bilioni 1.5, ambao pia unakabiliwa na ukosoaji wa kujikongoja, uzembe na kauli butu.
Soma pia:Duru zasema Afrika Kusini imetuma wanajeshi zaidi Kongo
Kabla ya mkutano huo mkubwa, viongozi hao watafanya kikao cha dharura siku ya Ijumaa kujadiliana machafuko huko Kongo, ambako waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameyakamata maeneo baada ya kuyashinda nguvu majeshi ya serikali.
Kulingana na Umoja huo, wakuu wote wa mataifa watahudhuria, ingawa haijulikani ikiwa Rais wa Rwanda Paul Kagame atakutana ana kwa ana na Felix Tshisekedi wa Kongo.