Mgawanyiko waibuka ndani ya chama cha SPLM-IO, Sudan Kusini
10 Aprili 2025Matangazo
Kuchaguliwa kwa Stephen Kuol Par, waziri wa Sudan Kusini wa kujenga amani, kama mwenyekiti wa muda wa chama hicho, kunafanyika siku mbili baada ya naibu wa chama hicho aliyekimbilia uhamishoni Oyet Nathaniel, kusimamisha uanachama wa Par na kumshutumu kwa kushirikiana na Rais Salva Kiir kuchukua nafasi yaMachar.
Wanachama wa chama hicho pia walionywa kutohudhuria mkutano huo wa Jumatano.
Par apuuzilia mbali kusimamishwa kwake
Par alipuuzilia mbali hatua ya kusimamishwa kwake na kuiita mzaha wa mwaka, huku akiongeza kuwa chama hicho hakiwezi kuongozwa au kuchukua amri kutoka kwa viongozi waliokimbilia uhamishoni.
Hata hivyo, amesema kuteuliwa kwake sio mapinduzi dhidi ya Machar, lakini ni njia ya kutatua mzozo wa uongozi wa chama hicho.