Mfungo wa Ramadhani waanza
1 Machi 2025Matangazo
Shirika la habari la Saudi Arabia lilichapisha kupitia mtandao wa X jioni ya Ijumaa (Februari 28) kwamba Mahakama ya Juu imeamua kwamba Jumamosi ndio siku ya mwanzo ya Ramadhani.
Algeria, Libya, Misri, Jordan, Palestina, Sudan, Lebanon na Tunisia nazo pia zimetangaza kuanza mfungo hivi leo.
Hata hivyo, ofisi ya kiongozi wa juu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, na ya ulamaa mkuu wa Iraq, Ayatullah Ali al-Sistani, zimetangaza kuanza mfungo siku ya Jumapili (Machi 2).
Mwezi huu mtukufu, ambapo mamilioni ya waumini kote duniani wanajizuwia kula, kunywa na mambo mengine wakati wa mchana, katika kutekeleza nguzo hiyo ya nne kati ya tano za dini ya Kiislamu. Inakadiriwa kuwa idadi ya waislamu imefikia bilioni 1.9 kote duniani.