UchumiKimataifa
Mfumuko wa bei kuendelea kuongezeka 2025
18 Agosti 2025Matangazo
Taasisi ya utafiti ya masuala ya uchumi ya Ujerumani ya Ifo, imebainisha kuwa mfumuko wa bei duniani unatarajiwa kuendelea kuwa juu kwa asilimia 4 mwaka huu. Kulingana na utafiti wa taasisi hiyo ongezeko kubwa zaidi la bei linatarajiwa kuikumba zaidi Afrika Mashariki na Afrika magharibi na kufikia asilimia 22.9 na asilimia 40.8.
Kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei kinatazamiwa kuwa asilimia 1.8 katika mataifa ya magharibi mwa Ulaya. Mtafiti wa taasisi hiyo Philipp Heil ameeleza kuwa mivutano ya kiuchumi na ushuru ndiyo sababu za ongezeko linalotarajiwa la mfumuko wa bei. Utafiti huo ulifanywa kati ya Juni 17 na Julai Mosi. Ulihusisha wataalamu 1,340 wa uchumi kutoka katika nchi 121 zilizohusishwa.