Mfumko wa bei umeendelea kupanda nchini Kenya
28 Februari 2025Mfumko wa bei nchini Kenya umepanda kwa mwezi wa nne mfululizo hadi kufikia wastani wa asilimia 3.5 mwezi Februari kutoka asilimia 3.3 mwezi Januari.
Hayo yametangazwa na ofisi ya takwimu nchini humo katika ripoti yake iliyotolewa leo Ijumaa. Mfumko wa bei ya bidhaa na huduma katika mwezi wa Februari ulibakia katika kiwango cha asilimia 2.0 mnamo mwezi Februari kiwango ambacho kilikuwa kinashuhudiwa tangu Januari,huku mfumko wa bei ya mahitaji yasiyokuwa ya kila siku, ukipanda hadi kufikia asilimia 8.2 katika mwezi wa Februari kutoka asilimia 7.1 mwezi uliotanguliwa.
Licha ya hali hiyo Benki Kuu ya Kenya ilitangaza kupunguza kiwango cha riba ya mikopo kwa mara ya nne mfululizo mnamo Febrauri 5 mwaka huu hadi kufikia asilimia 10.75. Chombo hicho kimesema hatua hiyo inalenga kuchochea uchumi licha wasiwasi kwamba kiwango cha chini cha riba kitachangia mfumuko wa bei za bidhaa na huduma.