Mfuko wa OPEC kuipatia Afrika dola bilioni 1
19 Juni 2025Matangazo
Msaada huo ni sehemu ya ahadi ya dola bilioni 2 iliyotolewa na nchi za Kiarabu kwa ajili ya kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mfuko huo wenye makao yake mjini Vienna, Austria, umetangaza Jumatano kiasi cha dola milioni 720 katika ufadhili mpya ili kusaidia juhudi za maendeleo barani Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Carribean, pamoja na kusainiwa kwa dola milioni 362 katika mikataba mipya ya mikopo.
Mikataba hiyo inahusisha mpango wa dola milioni 300 kwa Rwanda katika miaka mitatu ijayo, pamoja na mipango yenye thamani ya dola milioni 65 na dola milioni 40, kwa Ivory Coast na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki yenye makao yake makuu nchini Uganda.