MigogoroHaiti
Mfanyabiashara Laurent Saint-Cyr awa rais wa mpito, Haiti
8 Agosti 2025Matangazo
Kiongozi huyo mpya Saint- Cyr anaapa, huku kiongozi maarufu wa magenge hayo nchini humo akitishia kuipindua serikali.
Kwenye hafla ya uapisho iliyodhuriwa na mabalozi wa nchi kadhaa, Saint- Cyr alisema taifa hilo linapita kwenye mojawapo ya majanga makubwa zaidi kihistoria na kuongeza huu ni wakati wa kuchukua hatua.
Lakini saa chache kabla ya kuapishwa, Jimmy Chérizier "Barbecue", kiongozi wa muungano wenye nguvu wa magenge ya wahalifu alitishia kufanya mapinduzi, kufuatia madai ya muda mrefu kwamba serikali ya Haiti imejaa ukiritimba.