Lina Katuku ni msichana jasiri ambaye anajitolea kutoa elimu muhimu kuhusu hedhi salama kwa wasichana wa rika balehe. Kupitia juhudi zake, Lina anavunja vikwazo vya kijamii na aibu zinazozunguuka mada hii, akiwasaidia wasichana kuelewa mabadiliko ya mwili wao na jinsi ya kujitunza wakati wa hedhi.
Kipindi hiki kinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Msichana Jasiri ni muwazi, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!