Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ameingia kwenye muafaka mwengine wa kisiasa na mahasimu wake. Safari hii ikiwa ya nne, amesaini muafaka na Rais William Ruto, baada ya huko nyuma kuingia kwenye miafaka kama hiyo na Rais Daniel arap Moi, Rais Mwai Kibaki na Rais Uhuru Kenyatta.