Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kwa upande wa Bara, CHADEMA, kilihitimisha mkutano wake mkuu ambao kwa mara ya kwanza ndani ya miongo miwili umebadilisha uongozi wa juu wa chama hicho kutoka uwenyekiti wa Freeman Mbowe kwenda mikononi mwa aliyekuwa makamu wake, Tundu Lissu. Je, nini muelekeo wa CHADEMA hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.