SiasaUturuki
Meya wa Istanbul abakia rumande
20 Machi 2025Matangazo
Mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa nchini Uturuki Ekrem Imamoglu alikamatwa jana Jumatano siku chache kabla ya chama chake cha CHP kumtangaza kuwa mgombea wake wa kiti cha urais wa uchaguzi wa mwaka 2028.
Hatua hiyo imeyaporomosha masoko ya hisa nchini Uturuki na kuzusha lawama na ukosoaji kutoka kwenye chama chake ambacho kimeitisha maandamano makubwa mjini Istanbul.
Soma pia: Ocalan aitaka PKK kuweka chini silaha
Kiongozi wa chama cha CHP anatarajiwa kuwahutubia wafuasi wa chama hicho leo jioni huku wanafunzi wa vyuo vikuu wanapanga kuandamana mjini Istanbul kulaani kukamatwa kwa Imamoglu.
Hapo jana waandamanaji wenye hasira walikusanyika nje ya ofisi za mji huo wakipiga mayowe kumkosoa Rais Erdogan wakimwita "dikteta".