MEXICO CITY. Meya wa mji wa Mexico, Andreas Lopez, aungwa mkono na waandamanaji.
25 Aprili 2005Matangazo
Mamia ya maelfu ya raia wanafanya maandamano katika barabara za mji wa Mexico kumuunga mkono Andreas Manuel Lopez Obrador. Waandamanaji wanapinga kesi inayomkabili kiongozi huyo, ambayo huenda imzuilie kushiriki katika kuwania wadhifa wa rais katika uchaguzi wa rais mwaka ujao.
Bunge la nchi hiyo lilipiga kura kuruhusu mwanasiasa huyo kujibu mashtaka kuhusiana na kesi ya ardhi, hatua ambayo yeye mwenyewe ameilezea kuwa njama ya kisiasa dhidi yake.
Lopez ni mwanasiasa mashuhuri mwenye wafuasi wengi nchini Mexico. Kura ya maoni iliyofanywa hivi majuzi ilidhihirisha ushindi wa Lopez dhidi ya mgombea wa wadhifa wa urais anayeungwa mkono na rais Vicente Fox.