Merz kuzungumza na Trump,Zelensky kabla ya mkutano wa Alaska
12 Agosti 2025Matangazo
Katika mkutano huo, Merz atawashirikisha viongozi wengine wa Ulaya kutoka Ufaransa, Uingereza, Italia, Poland na Finland ili kujadiliana kuhusu masuala muhimu kabla ya mkutano wa kilele huko Alaska siku ya Ijumaa kati ya rais Donald Trump wa Marekani na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.
Wakati huo huo, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya walizungumza pia kwa njia ya video na kutoa wito wa kuendelea kuiunga mkono Ukraine na kuzidisha vikwazo kwa Urusi, huku wakisisitiza kushirikishwa kwa Ukraine na Ulaya kwenye mchakato wowote wa amani.
Hata hivyo Trump amesema usiku wa kuamkia leo kuwa mkutano wake na Putin haulengi kufikia makubaliano yoyote, bali ni wa kujadili namna ya kuvimaliza vita hivyo.