Fredrich Merz atetea mipango yake ya bajeti bungeni
13 Machi 2025Matangazo
Merz akitetea mipango yake ya bajeti ya matumizi katika kikao cha bunge leo amesema hatua za haraka zinahitajika kubadili sheria ya kuondowa ukomo wa serikali kukopa.Merz amesema.
"Tunapaswa kutazama baadae. Tunapaswa kutimiza wajibu huu na tunakabiliwa na hatua ya kufanya uamuzi wa kihistoria kwa nchi yetu'' Friedrich Merz alisema.
Soma pia:CDU/CSU na SPD kuanza mashauriano ya kuunda serikali
Muungano wa kihafidhina wa chama cha Merz ,cha CDU na chama ndugu CSU ambao wako kwenye mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na chama cha SPD, wanakimbizana na muda kulishinikiza bunge la sasa kupitisha mpango wa kufufua bajeti.