Merz asema yuko tayari kuwa Kansela wa Ujerumani
3 Februari 2025Matangazo
Merz anayekiongoza chama cha Christian Democratic Union (CDU) ametoa matamshi hayo wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika leo mjini Berlin, wiki tatu kabla ya kufanyika uchaguzi wa bunge wa Februari 23.
Amewaambia wajumbe waliokuwa wakimshangilia kwamba muungano wa vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU unaongoza kwenye uchunguzi wa maoni ya wapiga kura kwa sababu umedhihirisha unao "mpango kwa ajili ya Ujerumani."
Soma pia:Maelfu waandamana Ujerumani kupinga siasa kali
Merz ametoa matamshi hayo siku chache tangu alipozusha kizaazaa kufuatia uamuzi wake wa kukubali uungwaji mkono wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD kupitisha hoja bungeni ya kuzibana sheria za uhamiaji.