MigogoroUkraine
Merz: Vita vya nchini Ukraine "bado vingalipo"
22 Mei 2025Matangazo
Merz alisema mjini Berlin kwamba kwa sasa bado hakuna dalili kwamba vita hivyo vitamalizika mara moja.
Hata hivyo kansela huyo aligusia jitihada za kidiplomasia, akielezea uwezekano wa upatanishi kupitia Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni papa Leo akimtaja kama mwenye mamlaka ya mwisho ya kidunia.
Amesema inawezekana kukawa na matumaini kwamba angalau pande zinazozozana zinaweza kukutanishwa kwa ajili ya majadiliano yenye kujenga huko Vatican, na kwa upande mwingine akisisitiza umuhimu wa Ujerumani kujitoa zaidi kusaidia juhudi za amani.
Matamshi yake yanafuatia mazungumzo ya simu na Rais Donald Trump wa Marekani na Vladimir Putin wa Urusi.