Merz ana matumaini ya makubaliano kati ya EU na Marekani
9 Julai 2025Matangazo
Akizungumza bungeni, Merz amesema mwelekeo wa mazungumzo hayo unaashiria hatua chanya, ingawa bado kuna changamoto zinazopaswa kuzingatiwa.
Mataifa ya BRICS kukemea ushuru wa Trump
Naibu Kansela ambaye pia ni waziri wa fedha, Lars Klingbeil, ameitaka Marekani kukubali makubaliano ya ushuru wa haki na Umoja wa Ulaya, akionya kuwa kinyume chake kitasababisha hatua za kisasi kutoka kwa EU kulinda maslahi yake.
Merz aonya juu ya hatari ya ushuru wa Trump kwa uchumi wa Ujerumani
Akiwasilisha bajeti bungeni, Klingbeil alisisitiza kuwa makubaliano yoyote ya ushuru lazima yawe ya haki kwa pande zote, na akatoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kushirikiana kwa karibu ili kukabiliana na changamoto za kimataifa.