Merz amtembelea Macron
27 Februari 2025Ziara hiyo ya siku ya Jumatano (Februari 26) iliyoripotiwa na majarida ya Politico na Bild ilihusisha majadiliano juu ya mabadiliko ya hivi karibuni kwenye sera ya Marekani kuelekea vita nchini Ukraine, na pia uwezo wa Ulaya kujilinda.
Merz alichapisha kwenye mtandao wa X picha yake akiwa na Macron jioni ya Jumatano, akimshukuru kiongozi huyo wa Ufaransa kwa urafiki na imani yake kwenye mahusiano kati ya nchi zao jirani.
Soma zaidi: SPD tayari kwa mazungumzo ya 'dhati' na CDU
Hii ilikuwa ziara ya kwanza ya Merz nje ya nchi tangu muungano wake wa CDU-CSU kupata ushindi wa asilimia 28 kwenye uchaguzi wa Jumapili (Februari 23).
Majadililiano ya kuunda serikali ya mseto na chama cha SPD cha Kansela aliyeshindwa uchaguzi huo, Olaf Scholz, yalitarajiwa kuanza hivi punde.