Merz ampendekeza Klöckner kuwa Spika wa Bunge la Ujerumani
17 Machi 2025Matangazo
Merz ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kamati tendaji ya chama chake CDU mjini Berlin. Hata hivyo, wawakilishi wa chama hicho wameunga mkono ugombea wa Bi Klöckner anayetarajiwa kupigiwa kura katika kikao cha Bunge kilichopangwa kufanyika Machi 25.
Spika wa Bunge la Ujerumani ni cheo cha pili kwa ukubwa baada ya rais wa shirikisho, na kutokana na masuala ya itifaki wadhifa huo ni wa juu zaidi kuliko cheo cha Kansela.