Merz akaribia kushika usukani wa kuiongoza Ujerumani
28 Aprili 2025Matangazo
Hatua hiyo inamsogeza karibu zaidi na kuongoza taifa hilo, katikati ya mdororo wa uchumi, sera za kibiashara za Rais Donald Trump na vita vya nchini Ukraine.
Wajumbe katika kongamano la chama cha Merz cha Christian Democratic, CDU waliidhinisha makubaliano hayo yaliyofikiwa mapema mwezi huu, Shirika la habari la Ujerumani dpa liliripoti.
Hata hivyo, makubaliano hayo bado yanakabiliwa na kizingiti kikubwa kabla bunge halijakutana kwa ajili ya kumchagua Merz
Muungano huo wa serikali ya Merz unatarajiwa miongoni mwa mengineyo kuchochea ukuaji wa uchumi, kuimarisha matumizi ya ulinzi na kuimarisha za uhamiaji na kuendeleza mpango ulioachwa kwa muda mrefu wa maboresho ya Umoja wa Ulaya wenye mataifa zaidi ya 27.