Merz achukua mikoba ya Kansela wa Ujerumani
7 Mei 2025Amechukua wadhifa huo saa kadhaa baada ya kushindwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi wa awali uliofanyika ndani ya bunge majira ya asubuhi. Kwenye kura ya pili, Merz alichaguliwa kwa kura 325 katika bunge hilo la taifa, Bundestag, lenye viti 630.
Mwanasiasa huyo kutoka muungano wa vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU ataongoza serikali ya mseto na chama cha kansela aliyeondoka madarakani Olaf Scholz cha Social Democrats, SPD.
Kufuatia kuapishwa kwake, viongozi wa ulimwengu wamemtumia salamu za pongezi huku wengi kutoka barani Ulaya wakiahidi kufanya kazi kwa karibu na kansela huyo mpya.
Merz anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuukarabati uchumi unaojikokota, kutuliza mashaka ya umma juu ya sera ya uhamiaji na kurejesha nafasi ya Ujerumani kama taifa kiongozi ndani ya Umoja wa Ulaya.