Merkel: Ni vyema Papa ajaye akafuata mkondo wa Papa Francis
7 Mei 2025Matangazo
Merkel ameyasema haya Alhamis wakati ambapo makadinaliwanakutana huko Vatican kumchagua Baba Mtakatifu mpya wa kanisa hilo.
Kansela huyo wa zamani wa Ujerumani ambaye ni mtoto wa muhubiri wa Kiprotestanti, amekiambia kituo cha redio cha Kikatoliki mjini Cologne, Domradio kuwa, "itakuwa bora kama kutakuwa na mwendelezo."
Katika barua yake ya mwisho kwa maaskofu wa Kanisa Katoliki iliyochapishwa mnamo Oktoba mwaka 2024, marehemu Papa Francis aliandika kuhusiana na "upendo wa binadamu na kiroho wa moyo wa Yesu Kristo."
Na sasa Merkel mwenye umri wa miaka 70 anasema Baba Mtakatifu Francis alimkubali kila mmoja na alipendezwa sana na jambo hilo.