Merkel aunga mkono haki ya Israel kujilinda
21 Juni 2025Matangazo
Katika taarifa yake iliyochapishwa leo na gazeti la Neue Osnabrücker, Merkel amesema ikiwa baadhi ya watu wanaruhusiwa kutangaza kwamba wanataka kuliangamiza taifa la Israel, basi taifa hilo lazima liweze kujilinda.
Merkel alaani mashambulizi dhidi ya Israel
Akizungumzia wasiwasi kuhusu iwapo hatua za Israel zinazingatia sheria ya kimataifa, Merkel amesema wakati uwepo wa nchi unatiliwa mashaka na Hamas au Iran, hauwezi moja kwa moja kujibu hilo chini ya sheria za kimataifa.
Kinyume chake, Merkel amesema hali ya vita vya Ukraine iko wazi kabisa. Amesisitiza kuwa shambulizi la Urusi dhidi ya Ukraine ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa na kuongeza kuwa Ukraine haijawahi kuitishia Urusi lakini ilishambuliwa.