Matangazo
Meneja anayesimamia idara ya teknolojia na mawasiliano katika tume huru inayosimamia uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC) Chris Musando, amepatikana amefariki. Haya yanajiri siku tatu baada ya meneja huyo kutoweka. Kadhalika yanajiri ikiwa zimesalia siku saba tu Kenya ifanye uchaguzi wake mkuu utakaofanyika Agosti nane. Kabla ya mwili wake kupatikana, Idhaa ya Kiswahili ya DW ilizungumza na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati na haya ndiyo aliyoyasema alipohojiwa na mwanahabari Lillian Mtono.