Meloni apinga kuitambua Palestina kabla ya kuundwa rasmi
26 Julai 2025Matangazo
Meloni ameliambia gazeti la kila siku la nchini Italia, "La Repubblica" kwamba anaunga mkono kikamilifu kuundwa kwa dola huru ya Palestina lakini hakubaliani na njia ya kuitambua kabla ya kuanzishwa rasmi.
Amesema njia hiyo ya kuitambua Palestina kupitia makaratasi pekee inatengeeza fikra ya kuwa tatizo lililopo limetatuliwa, kinyume kabisa na uhalisia.
Matamshi hayo ameyatoa baada ya Ufaransa kutangaza wiki hii nia yake ya kulitambua rasmi taifa la Palestina ifikapo mwezi Septemba.
Uamuzi huo uliokosolewa vikali na Israel na Marekani, umetangazwa katika wakati shinikizo la kimataifa linaongezeka kutaka vita vya Gaza vikomeshwe.