Meloni achunguzwa kuhusu kuwachiwa mbabe wa kivita wa Libya
29 Januari 2025Mwanasiasa huyo wa mrengo wa kulia ametangaza habari hizo mwenyewe katika ujumbe wa video uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii. Amesema anachunguzwa kwa madai ya kusaidia kumtorosha mshukiwa wa uhalifu wa kivita.
Osama Almasri Najeem, mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai ya Libya, aliachiwa wiki iliyopita baada ya kukamatwa mjini Turin siku chache kabla, kufuatia waranti wa ICC kuhusu uhalifu wa kivita.
Mahakama ya ICC yenye makao makuu yake mjini The Hague imesema haikufahamishwa kuhusu kuwachiwa kwa mshukiwa huyo na kwa hiyo inataka ufafanuzi kutoka kwa Italia. Serikali ya Meloni imekosolewa tangu Mlibya huyo alipoachiwa, ambaye pia ni mkuu wa 0jela moja ya mji mkuu wa Libya Tripoli. Ripoti kadhaa za vyombo vya habari zilisema Almasri Najeem alisafirishwa hadi Tripoli katika ndege ya serikali ya Italia.