MigogoroMashariki ya Kati
Meli ya chakula cha Gaza yatia nanga Israel
20 Agosti 2025Matangazo
Meli hiyo inayopeperusha bendera ya Panama iliondoka Cyprus siku ya Jumatatu ikiwa na tani 1,200 za tambi, mchele, lishe ya watoto na vyakula vingine vya kusindikwa.
Shehena hiyo ya misaada itaaanza kusambazwa leo kwenye Ukanda wa Gaza eneo ambako mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema ukosefu wa chakula umefikia kiwango kisicho mithili.
Msaada huo umewasili siku moja baada ya kundi la Hamaskuridhia pendekezo jipya la kusitisha vita lililotolewa na wapatanishi wa nchi za kiarabu. Hata hivyo hadi sasa Israel haijatoa majibu kuhusu pendekezo hilo la kusitisha mapigano kwa muda wa siku 60.