Meli iliyobeba bidhaa hatari yazama kusini mwa Bahari Hindi
25 Mei 2025Matangazo
Taarifa ya jeshi la wanamaji la India imefahamisha kwamba mabaharia wote waliokuwamo kwenye meli hiyo wameokolewa.
Jeshi hilo limesema meli hiyo kwa jina MSC ELSA 3 ilikuwa inasafiri kutoka bandari ya India ya Vizhinjam kuelekea Kochi ilipata hitilafu siku ya Jumamosi na kuwasiliana nao.
Wizara ya Ulinzi ya India ilithibitisha kuokolewa kwa mabaharia hao 24 ambao wengi wao wanadaiwa kutokea Georgia, Urusi, Ukraine na Ufilipino.
Kontaina 640 zilikuwepo katika meli hiyo, ikiwemo 13 zilizoandikwa mzigo hatari na 12 zikiwa na madini ya Calcium carbide. Hakuna taarifa zozote hadi sasa kuhusu mzigo uliokuwa ndani ya makonteina hatari.